banner

June 22, 2021

BERNARD MORRISON AOMBA KUKUTANA NA SHABIKI ALIYETEMBEA KWA MGUU KUTOKA KIGOMA

BERNARD MORRISON AOMBA KUKUTANA NA SHABIKI ALIYETEMBEA KWA MGUU KUTOKA KIGOMA

 


NYOTA wa Simba, Bernard Morrison ameomba kukutana na shabiki wa timu hiyo Michael Filbert ambaye ametembea kwa miguu kutoka Kigoma mpaka Dar es Salaam. 


Sababu kubwa ya shabiki huyo kufanya hivyo ni kwa ajili ya kushuhudia mchezo wao dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa. 

Juni 21 Michael aliwasili Dar baada ya kutumia siku 15 na alipokelewa na mashabiki wa Simba na kundi la Simba Ushirikiano kutoka Kigogo.

Kupitia Ukurasa wa Instagram wa Mwandishi wa EATV, Zainabu Rajabu baada ya kuposti habari ya shabiki huyo kutua Bongo, Morrison aliandika:"Nahitaji kumuona yeye katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo wa leo tafadhali,".

Leo Juni 22, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search