banner

October 27, 2021

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 27.10.2021: Pogba, Rodgers, Ten Hag, Klopp, Saliba, Alvarez, Dembele

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 27.10.2021: Pogba, Rodgers, Ten Hag, Klopp, Saliba, Alvarez, Dembele


Kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 28, alimpuuza kocha Ole Gunnar Solskjaer baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika kichapo cha 5-0 dhidi ya Liverpool Jumapili na mfaransa huyo amesimamisha mazungumzo ya mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo. (Sun)


Man United ina orodha ya majina manne ya kumrithi kocha wake aliyekalia kuti kavu Solskjaer, akiwemo Zinedine Zidane, Antonio Conte, Meneja wa Leicester Brendan Rodgers na wa Ajax boss Erik ten Hag. (Sun)


Lakini Meneja wa Paris St-Germain Muargentina Mauricio Pochettino, 49, anasalia kuwa chaguo namba moja la Manchester United kumrithi Solskjaer. (Star)


Newcastle wako tayari kumpa Ten Hag mshahara wa £6m kwa mwaka baada ya kodi na kufanya marupurupu yote kufikia £11m kwa mwaka lakini Mholanzi huyo, 51, amegoma kuondoka Ajax. (Mail)


Newcastle pia haijakata tamaa kumrejesha kocha wake wa zamani Rafael Benitez. Mhispania huyo, 61, kwa sasa anainoa Everton. (Football Insider)

b

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Rafael Benitez

Meneja wa zamani wa Roma Paulo Fonseca, 48, anatarajia kukubali ofa ya kuwa Meneja mpya wa Newcastle, lakini wamiliki wapya wa klabu hiyo bado wanatafakari uamuzi wao. (Fabrizio Romano, via Chronicle)

Barcelona bado wanamatumini ya kumpata kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp, 54, ili amrithi kocha wa sasa Ronald Koeman. (Sport - in Spanish)

Arsenal inahaha kumshawishi William Saliba kwamba maisha yake ya soka ni pale Emirates na wanaweza kulazimika kumuuza mlinzi huyo mfaransa, 20, ambaye ameonyesha kiwango cha kuvutia Marseille anapocheza kwa mkopo. (Sun)

Arsenal wanajiandaa kupambana na Manchester City katika mbio za kumsajili kama mchezaji huru mlinzi wa Hispania Sergi Roberto, 29 kutoka Barcelona . (Fichajes, via talkSPORT)

v

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Sergi Roberto

Kiungo wa Manchester United Donny van de Beek amemkataa wakala wa soka Mino Raiola baada ya wakala huyo kumuomba mholanzi huyo mwenye miaka 24 awe wakala wake mpya. (Mike Verweij, via Express)

Chelsea imepewa ofa ya kumsajili mlinzi wa Uholanzi mwenye miaka 22 Matthijs de Ligt wakati huu Juventus ikitaka kupunguza kiwango cha mishahara inayotoa kwa wachezaji. (Goal, via Star)

Aston Villa, AC Milan na Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mshambuliaji wa River Plate Muargentina Julian Alvarez, 21. (CalcioMercato - in Italian)

Barcelona imemfahamisha winga wake Mfaransa Ousmane Dembele, 24, kwamba ana mwezi mmoja tu wa kukubali ofa yao mpya ya kuongeza mkataba wake wa sasa ambao unakoma mwishoni mwa msimu ujao.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search