banner

April 01, 2023

NABI AWATUMIA TP MAZEMBE KUWACHAKAZA SIMBA

NABI AWATUMIA TP MAZEMBE KUWACHAKAZA SIMBA



Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefichua kuwa amepanga kuutumia mchezo wao dhidi ya TP Mazembe kufanya maandalizi ya mchezo wao na Simba katika Ligi Kuu Bara unaotarajia kupigwa Aprili 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa.


Kesho Jumapili Yanga itashuka kwenye Uwanja wa TP Mazembe uliopo Lumbumbashi nchini DR Congo kukamilisha ratiba ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya kurejea nchini kuwavaa Geita Gold katika mchezo wa Kombe la FA utakaopigwa Aprili 8, mwaka huu.


Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa wanakwenda kucheza na TP Mazembe kwa lengo la kutafuta matokeo ya heshima kabla ya kucheza na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao kwao matokeo ya ushindi ni jambo la muhimu.



“Hatua ya kwanza, tumefanikiwa kwa sababu tumeshafuzu hatua ya robo fainali katika michuano hii ya Shirikisho Afrika hivyo tunaenda kwa ajili ya kutafuta matokeo ya heshima ili kubakia kuwa juu katika kundi ingawa haitokuwa mechi nyepesi kwa sababu wao wanapitia kipindi kigumu msimu huu katika haya mashindano.


“Ugumu wa mchezo huu kwetu ni sehemu ya maandalizi ya mechi zetu mbili za ndani, tuna mchezo wa nusu fainali ya FA dhidi ya Geita Gold lakini tuna mchezo mwengine mgumu dhidi ya Simba katika Ligi Kuu Bara ambayo yote ukiangalia kwetu ina umuhimu wa kuweza kupata matokeo ya ushindi na huu mchezo wetu wa DR Congo utatupa mwanga, “ alisema Nabi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search