banner

July 07, 2016

KENYA : MWANAFUNZI AJIUA BAADA YA KUSHINDWA KWENYE MCHEZO WA KUBASHIRI (BETTING)

KENYA : MWANAFUNZI AJIUA BAADA YA KUSHINDWA KWENYE MCHEZO WA KUBASHIRI (BETTING)

Mwanafunzi mmoja kutoka katika kaunti ya Migori nchini Kenya amejinyonga hadi kufa baada ya kupoteza fedha zake katika mchezo wa kubashiri (betting).
Mwanafunzi huyo kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta alijiua siku ya Jumatano Julai 6 baada ya kupoteza KSh 80,000 alizotumia kwenye mchezo wa kubashiri kati ya Ujerumani na Italia ambao ulikuwa ni mchezo wa robo fainali ya EURO2016.
Mwanafunzi huyo aliweka Ksh 40,000 kwa upande wa Ujerumani kuwa itashinda lakini pia akaweka kiasi hicho hicho kwa upande wa Italia kuwa itashinda katika muda wa kawaida (dakika 90).
Baada ya kushindwa kwani timu hizo zilikwenda hadi hatua ya kupigiana penati, mwanafunzi huyo alisafiri hadi kijijini kwao ambapo alijinyonga na aliacha ujumbe ulioelezea sababu ya kufanya hivyo kuwa ni baada ya kupoteza fedha alizopewa kwa ajili ya ada.

Bofya HAPA Ku-install App ya Ruwehy Official ili usi sumbuke kuingia kwenye website.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search