Mshambuliaji wa Barcelona Neymar Da Silva Santos anatamani kucheza katika ligi kuu nchini Uingereza ambapo alihusishwa na Manchester United katika usajili uliopita wa majira ya joto.
“Navutiwa na Manchester United, Liverpool, Arsenal na Chelsea, siku zote klabu hizi zimekuwa zikigombea ubingwa na kuna makocha kama Pep Guardiola na Jose Mourinho mchezaji yoyote angependa kucheza chini ya makocha hao.Nani anajua?, Ningependa kucheza huko,” alisema Neymar.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa juu ya tetesi za Mourinho kuwasiliana na Mbrazil huyo kwa siri akimshawishi mshambuliaji huyo kutumkia Old Trafford.
Post a Comment