banner

March 17, 2017

SINGIDA: POLISI ALIYEKUWA AKIJIHAMI AMUUA RAIA

SINGIDA: POLISI ALIYEKUWA AKIJIHAMI AMUUA RAIA

Mkazi wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Herman Joseph(32), anayedaiwa kujihusisha na uhalifu alikufa baada ya kupigwa risasi tumboni na askari polisi aliyekuwa akijihami.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba anasema tukio hilo lilitokea juzi alasiri eneo la Ikungi madukani ambapo marehemu Herman Joseph(32) alikuwa akigombana na mkewe Maria Jacob(28) hali iliyosababisha mwanamke huyo kujeruhiwa na kisu kwenye makalio kabla ya marehemu kumjeruhi pia kwa kisu tumboni Janeth Mathias(28).
Baada ya majeruhi kupiga yowe wananchi walifika katika eneo hilo ambapo Shaban Jumanne (35) nae alijeruhiwa mkono wa kulia na Issa Shaban(48) mkono wa kushoto. Huku akijigamba kuwa haogopi chochote na hakuna atakayeweza kumkamata.
“Baada ya Taarifa kufika katika kituo kidogo cha polisi Ikungi, askari wanne walifika eneo la tukio” alisema.
Askari walipofika eneo la tukio walimkuta Joseph na kumtaka ajisalimishe, ila hakutii na kuanza kumfuata askari huku akiwa na kisu chake mkononi kwa lengo la kumchoma askari kifuani. Askari aliyekuwa na silaha alifyatua risasi mbili hewani huku akirudi nyuma ili kumfanya Herman aogope.
Alifafanua kuwa wakati askari akijaribu kujihami kwa kurudi kinyumenyume, alijikwaa na kuanguka chini. ndipo marehemu alipotaka kumchoma kisu kifuani lakini  aliwahiwa kwa kupigwa risasi tumboni na kupelekea kifo chake.
Kutokana na tukio hilo, Kamanda Magiligimba alisema polisi inaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli halisi na hatimaye haki kutolewa kulingana na majibu ya upelelezi mzima wa tukio.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search