banner

April 28, 2017

AZAM: HILI NDIO KOMBE LETU, SIMBA WATUSAMEHE TU

AZAM: HILI NDIO KOMBE LETU, SIMBA WATUSAMEHE TU

BAADA ya kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Azam FC imeelekeza nguvu kwenye michuano ya kombe la FA na wataanza kesho kwenye mchezo dhidi ya Simba.
Azam kesho itakuwa mgeni wa Simba katika mchezo wa nusu fainali utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Wanalambalamba hao wakiwa wamejipanga kuibuka na ushindi ili kutinga fainali na kuchukua ubingwa ikiwa ndio njia pekee ya kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwavile hawapo kwenye mbio za ubingwa wa Vodacom.
Jaffar Idd, Afisa Habari wa Azam FC
Ofisa habari wa klabu hiyo Jaffar Idd amesema kuwa michuano pekee wanayoichukulia kwa uzito ni hiyo kwakuwa ndiyo yenye kibali cha kuipeleka kucheza kombe la Shirikisho Afrika.
“Mchezo utakuwa mgumu, Simba tunaiheshimu ina wachezaji wazuri na tuliwafunga katika michezo miwili iliyopita, nina imani watakuja kwa dhamira ya kulipa kisasi ila nasi tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michuano hii tukianza na mchezo wa kesho,” alisema Jaffar.
Jaffar alisema klabu yake inawataka waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo huo kufuata sheria 17 za soka ili mshindi apatikane kwa haki bila ya malalamiko yoyote.
Wakati huo huo Jaffar alisema nahodha wao John Bocco anaweza kucheza au kutocheza kwenye mchezo huo kulingana na maamuzi ya kocha Aristica Cioba kwani ameanza mazoezi na wenzake baada ya kupona majeruhi.
BOIPLUS MEDIA

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search