banner

May 10, 2017

ATLETICO YASHINDA 2-1, REAL MADRID YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

ATLETICO YASHINDA 2-1, REAL MADRID YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itapigwa Juni 3, mwaka huu jijini Cardiff na itawakutanisha Juventus dhidi Real Madrid.

Madrid imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid leo. Lakini imefuzu kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya ushindi wa 3-0 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mabao ya Atletico Madrid yamefungwa na Saul na Antoinne Griezmann na lile la Madrid likafungwa na Isco.

Kumbuka Juventus wamefuzu kwa kuiondoa AS Monaco ya Ufaransa na sasa ni fainali ya vigogo na wakongwe kutoka Hispania na Italia.




Atletico Madrid starting XI: Oblak, Gimenez, Savic, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Saul, Carrasco, Torres, Griezmann 
Subs: Miguel Moya, Tiago, Correa, Lucas, Gameiro, Thomas, Gaitan 

Real Madrid starting XI: Navas, Danilo, Sergio Ramos, Varane, Marcelo, Kroos, Casemiro, Modric, Isco, Benzema, Ronaldo 
Subs: Casilla, Nacho, Rodriguez, Kovacic, Lucas, Marco, Morata
























Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search