banner

June 20, 2017

KOCHA JOSE MOURINHO KITANZINI, ADAIWA KUKWEPA KODI

KOCHA JOSE MOURINHO KITANZINI, ADAIWA KUKWEPA KODI

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ametuhumiwa kufanya ulaghai wakati wa ulipaji kodi alipokuwa katika Klabu ya Real Madrid.
Maofisa wa mashtaka nchini humo wanasema alitenda makosa hayo alipokuwa akiinoa Real Madrid, ambapo jumla imeelezwa kuwa amekwepa kulipa kodi ya pauni milioni 2.9 ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 6 kati ya mwaka 2011 na mwaka 2012.
Watu wengine mashuhuri katika soka ambao wametuhumiwa kufanya ulaghai wakati wa kulipa kodi nchini Hispania ni pamoja na nyota wa Barcelona, Lionel Messi ambaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 jela, hata hivyo Messi, hatarajiwi kwenda jela.
Hivi karibuni nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo naye aliingia kwenye kashfa ya kukwepa kodi na inaelezwa kuwa alikwepa zaidi ya pauni milioni 12 ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 33 lakini mwenyewe alikanusha madai hayo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search