banner

June 05, 2017

MASKINI JAMES RODRIGUEZ NDANI YA REAL MADRID

MASKINI JAMES RODRIGUEZ NDANI YA REAL MADRID

Licha ya kushuhudia timu yake ya Real Madrid ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, bado straika wa timu hiyo, James Rodriguez ameonyesha hana furaha klabuni hapo.
Mchezaji huyo hakuwepo hata benchi katika mchezo huo wa fainali ya Jumamosi ambapo kikosi cha Kocha Zinedine Zidane kilipata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Juventus.

Baada ya ushindi huo Rodriguez aliingia uwanjani akiwa na jezi kisha akawa anatabasamu huku ameshika kombe lakini hakupiga picha nyingi akaondoka na pia ndiye alikuwa mchezaji wa kwanza kuingia kwenye basi la wachezaji wa Real Madrid wakati wa kuondoka akionekana kuwa mnyonge.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search