banner

August 14, 2017

CRISTIANO RONALDO HATARINI KUFUNGIWA MECHI 4 HADI 12

CRISTIANO RONALDO HATARINI KUFUNGIWA MECHI 4 HADI 12

Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo yupo hatarini kufungiwa kutocheza katika mechi nne hadi 12 kuokana na kitendo chake cha kumsukuma mwamuzi wakati wa mchezo wa Supercopa de Espana dhidi ya Hispania, usiku wa kuamkia leo.
Ronaldo ambaye alifunga bao moja katika kipute hicho dhidi ya Barcelona, alipewa kadi nyekundu baada ya kujiagusha ndani ya eneo la wapinzani na ndipo mwamuzi akampa kadi ya pili ya njani lakini wakati akilalamika, alimsukuma mgongoni.
Katika mchezo huo ambao Real Madrid walipata ushindi wa mabao 3-1 inaonyesha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 96 cha kanuni za soka za Chama cha Soka cha Hispania kitendo cha kumsukuma mwamuzi kinaweza kumfanya mchezaji afungiwe mechi nne hadi 12.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search