banner

October 15, 2019

KOCHA WA AZAM FC AWACHANA WACHEZAJI WAKE LICHA YA USHINDI WA MABAO 2-0

KOCHA WA AZAM FC AWACHANA WACHEZAJI WAKE LICHA YA USHINDI WA MABAO 2-0


LICHA ya Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Africn Lyon, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa bado wachezaji wake walipuuzia mchezo.

Azam FC ilicheza jana uwanja wa Uhuru na kuibuka wababe mbele ya African Lyon kwenye mchezo wa kujipima nguvu.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Idd Kipagwile pamoja na Joseph Mahundi.

"Wachezaji wangu ilifika wakati waliudharau mchezo, tulianza kwa kasi kipindi cha kwanza ila wachezaji 'warilelax' kwa muda mrefu.

"Tulikuwa na nafasi ya kushinda kwa mabao mengi ila umaliziaji ulikuwa ni tatizo jambo ambalo limetufanya tupate ushindi mdogo," amesema.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search