banner

October 11, 2019

NI BALAA LINGINE! WASHINDI WA SIMU JANJA WAENDELEA KUFURAHIA HUDUMA ZA SPORTPESA

NI BALAA LINGINE! WASHINDI WA SIMU JANJA WAENDELEA KUFURAHIA HUDUMA ZA SPORTPESA


Washindi wa promosheni ya Faidika na Jero inayoendeshwa na kampuni ya mtandao wa Tigo kwa kushirikiana na SportPesa waendelea kufurahia huduma mbalimbali huku wakipata nafasi ya kujishindia simu na hatimaye gari kwenye droo ya mwisho inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2019.

Wiki iliyopita SportPesa ilitangaza washindi saba kutoka mikoa mbalimbali ambapo washindi watatu wakitokea Dar es Salaam na wikii hii SportPesa imetangaza washindi wengine saba wanne wakitokea jijini Dar es Salaam.

Washindi wa wiki hii kutoka DSM ni Farid Ismail Ally kutoka Temek, Ibrahim Mudi Kubamba kutoka Ilala, Mfaume Enzi Kungulilo kutoka Mbezi na Mecklord Smith Kamnde  kutoka Tabata Segerea.

Kutoka mikoa mingine ni Said Selemani Navake kutoka Mtwara, Salumu Gustafu Andrew kutoka Morogoro na Erick Hassan Kiwala kutoka Iringa.

Promosheni bado inaendelea ambapo mtumiaji wa mtandao wa Tigo kwa kupitia huduma ya Tigopesa anaweza kujisajiri, kuweka pesa na kucheza/kuweka ubashiri wake utakaompelekea kuingia kwenye droo ya kujishindia simu kila siku na gari aina ya Renault Kwid mwisho wa promosheni.

Akizungumza wakati wa makabidhiano Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Bwana Tarimba Abbas alisema tunafuraha sana kuona tunapata washindi kutoka sehemu mbalimbali nchini na wanafurahia sana mara wanapokabidhiwa zawadi zao.

“Wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja hivyo basi sisi kama SportPesa tunapenda kuwajulisha wateja wetu kwamba tunawajali na kuwathamini maana sisi kwetu mteja ni mfalme.

Huduma zetu ni saa 24 siku 7 za wiki kuhakikisha wahuduma wetu zaidi ya 100 wanasikiliza matatizo na mahitaji ya wateja.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search