banner

April 04, 2020

GALLAS: NINAWEZA KUCHEZA NDANI NA NJE YA BONGO

GALLAS: NINAWEZA KUCHEZA NDANI NA NJE YA BONGO


WILLIAM Lucian, ‘Gallas’ beki wa kuliwa wa Polisi Tanzania amesema kuwa ana uwezo wa kucheza popote ndani ya Bongo na nje pia.
Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 29 ina pointi 45 imefunga mabao 29 na safu ya ulinzi imeruhusu mabao 26, kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Gallas amesema kuwa hana mashaka na uwezo wake inapofika suala la kucheza jambo linalomfanya kujiamini.
“Nina uwezo wa kucheza ndani ya Bongo na nje ya nchi kwa kuwa mimi ni mchezaji na ninatambua namna ya kulinda kipaji changu, sina tatizo nikiwa ndani ya uwanja kwa kuwa ni muhimu kufanya vizuri.
“Nimecheza timu nyingi kwa kuwa ninaweza kuwa bora katika kazi yangu ambayo ninaifanya, siogopi na ninajiamini muda wote," amesema.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search