banner

April 22, 2017

MASHABIKI 7 WAFARIKI DUNIA WAKIANGALIA MCHEZO WA MAN UNITED V ANDERLECHT

MASHABIKI 7 WAFARIKI DUNIA WAKIANGALIA MCHEZO WA MAN UNITED V ANDERLECHT

Mashabiki 7 wa soka nchini Nigeria wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa kufuatia hitilafu ya umeme iliyotokea jirani na kibanda walichokuwa wakitazama mchezo wa Europa League kati ya Manchester United na Anderlecht.
Taarifa kutoka katika mji wa Calabar lilipotokea tukio hilo zinadai kuwa, mashabiki hao wa mpira walikumbwa na mkasa huo baada ya kibanda walichokuwamo ndani kuangukiwa na transifoma pamoja na nguzo ya umeme na hivyo kusababisha shoti kubwa.
Baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa, kulikuwa na watazamaji wa mpira 80 ndani ya kibanda hicho ambapo wengine waliweza kutoka salama.
Shabiki mmoja miongoni mwa waliopelekwa hospitali yupo katika hali mbaya.
Katika mchezo huo, Manchester ilifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Anderlecht kwa jumla ya magoli 3-2.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search