banner

April 24, 2024

YANGA NA TABORA MEI MOSI CRDB BANK FEDERATION CUP

YANGA NA TABORA MEI MOSI CRDB BANK FEDERATION CUP



MABINGWA watetezi, Yanga SC watamenyana na Tabora United Mei 1 katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia Saa 2:30 usiku.
Mchezo huo utatanguliwa na michezo miwili siku hiyo ya Robo Fainali ya CRDB Bank Federation Cup kati ya Ihefu SC na Mashujaa Saa 10:00 jioni Uwanja wa LITI mjini Singida na Coastal Unión dhidi ya Geita Gold Saa 12:15 jioni Uwanja wa  Mkwakwani Jijini Tanga.
Hatua ya Robó Fainali ya CRDB Bank Federation Cup  itakamilishwa Mei 3 kwa mchezo kati ya Azam FC na Namungo FC Saa 1:00 usiku Uwanja Azam Complex.


source http://www.binzubeiry.co.tz/2024/04/yanga-na-tabora-mei-mosi-crdb-bank.html

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search