Bin RUWEHY inakuletea muhtasari wa tetesi na habari za uhamisho kutoka Ligi Kuu Uingereza, La Liga, Serie A, Bundesliga na kwingineko
REAL MADRID WAINGILIA DILI LA ARSENAL KUMSAJILI MBAPPE, DAU LAKE LAPANDA
Wakati usajili ukiendelea, Klabu ya Arsenal ina hofu kuwa inaweza ikamkosa mshambuliaji chipukizi wa Monaco, Kylian Mbappe amabyo inamuwania kwa kuwa mchezaji huyo naye anawaniwa na wababe wa Hispania, Real Madrid.
Arsenal imetajwa kuwa inamuwani mchezaji huyo aliyeonyesha uwezo wa juu msimu uliopita lakini kuingia kwa Real Madrid kumesababisha dau la mchezaji huyo kupanda na sasa anaweza kuuzwa kwa pauni milioni 87.
Mbali na Madrid, Mbappe ambaye ana umri wa miaka 18, pia anawaniwa na klabu nyingine kubwa za Ulaya.
Mbali na Madrid, Mbappe ambaye ana umri wa miaka 18, pia anawaniwa na klabu nyingine kubwa za Ulaya.
FELLAINI AZUNGUMZIA KUHUSU KUYAFUATA MABILIONI YA WACHINA, ASEMA INAWEZEKANA
Kiungo Marouane Fellaini ameshindwa kukataa taarifa zinazomhusisha yeye kuihama timu yake ya Manchester United ili kwenda China kucheza soka.
Fellaini amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Kocha Jose Mourinho licha ya kuwa awali alionekana kama amekosa mwelekeo mzuri klabuni hapo.
Amesema hayo alipoulizwa juu ya majaaliwa yake kwa kusema: “Kwenda China? Kwa nini isiwezekane?
"Mimi bado ni mchezaji wa Manchester United lakini siwezi kukataa ofa nzuri inapokuja.
Amesema hayo alipoulizwa juu ya majaaliwa yake kwa kusema: “Kwenda China? Kwa nini isiwezekane?
"Mimi bado ni mchezaji wa Manchester United lakini siwezi kukataa ofa nzuri inapokuja.
Kwa miaka ya hivi karibuni klabu za China zimekuwa zikitoa madau manono kwa wachezaji wa Ulaya hasa wale wenye majina makubwa na baadhi yao wameshakimbilia kucheza soka nchini humo wakiwemo Hulk, Carlos Tevez na Oscar.
KOCHA WA MARIO BALOTELLI, ATUA URUSI, ALAMBA MIAKA MIWILI
Klabu ya Zenit St Petersburg ya Urusi imemteua aliyekuwa kocha wa Manchester City, Roberto Mancini kuwa kocha wao mkuu kwa kumpa mkataba wa miaka mitatu.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Italia ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 52, anachukua nafasi ya Mircea Lucescu aliyefutwa kazi wiki iliyopita baada ya kuwa kwenye usukani kwa msimu mmoja.
Zenit walimaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Urusi na kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mancini ambayenio kocha wa straika Mario balotelli, aliyeshinda Ligi ya Premier League akiwa na Manchester City mwaka 2012, alikuwa kocha wa Inter Milan lakini akaondoka mwaka 2016.
Katika mkataba huo wa sasa wa Klabu ya Zenit, ana nafasi ya kuongeza mkataba wake kwa miaka mingine miwili.
PEPE ‘BEKI KATILI’ BASI TENA, ANAONDOKA REAL MADRID
Wakati Real Madrid ikishuka uwanjani kuivaa Juventus katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumamosi hii upande mwingine ni kuwa beki mkongwe wa Madrid, Pepe ataondoka mara baada ya fainali hiyo.
Pepe ambaye amedumu kikosini hapo kwa misimu tisa, alikuwa hajatamka wazi juu ya mwelekeo wake.
Nafasi ya Pepe ndani ya Madrid kwa sasa inaonekana kushikiliwa na Raphael Varane raia wa Ufaransa.
Pepe ambaye ana umri wa miaka 34, alisajiliwa klabuni hapo mwaka 2007 kwa euro milioni 30 na hapo kati aliwahi kuwania na klabu nyingine kadhaa ikiwemo Manchester City.
BARCA YATETA NA SEMEDO KWA HERUFI KUBWA
Barcelona wapo katika mazungumzo yaliyochangamka na Nelsen Semedo wa Benfica, kwa mujibu wa Record .
Semedo anaweza kupatakana kwa paundi milioni 69 kama bei iliyopangwa na klabu yake, lakini Barca wanakaribia kumnasa kwa paundi milioni 43.
MAN UTD YAANDAA DAU LA PERISIC
Manchester United wapo tayari kutoa dau la euro milioni 52 kwa ajili ya winga wa Inter Milan Ivan Perisic, Gazzetta dello Sport limeripoti.
United wanataka kuimarisha zaidi na kukifanya kipana kikosi chao na tayari wameshatenga dau la euro milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia.
LIVERPOOL YAWANYATIA SALAH & BALDE
Liverpool bado wanaendelea na mazungumzo katika mchakato wao wa kuifukuzia saini ya Mohamed Salah kutoka Roma, pia wanavutiwa na Kieta Balde Diao kutoka Lazio, kwa mujibu wa ESPN .
CHELSEA WANAMTAKA ALVES
Chelsea, Manchester City na Tottenham wanafikiria kumsajili Dani Alves majira ya joto, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mbrazili huyo anaaminika kuwa tayari kuondoka Juventus mwisho wa msimu huu, Conte akiwa shabiki wake mkubwa anataka kumleta Darajani ampe changamoto Victor Moses.
ARSENAL YAJIUNGA MBIO ZA MBAPPE
Arsenal nayo imeingia kwenye mbio za kuifukuzia saini ya nyota wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa L'Equipe .
Kinda huyo amezivutia klabu nyingi Ulaya, Real Madrid na Manchester United zikiwa klabu zenye nafasi kubwa zaidi kuinasa saini yake.
Lakini Arsene Wenger akiwa amesaini mkataba mpya tena, Gunners wapo tayari kutoa hadi euro milioni 100 kumleta nyota huyo kinda uwanja wa Emirates.
REAL MADRID YAANDAA £100M KUMSAJILI HAZARD
Real Madrid wamejiandaa kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kumsajli Eden Hazard kutoka Chelsea, kwa mujibu wa the Sun .
Miamba hao wa La Liga tayari wameshakutana na wawakilishi wa Hazard mara tatu katika harakati zao kumsajli mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kwa ada ya hatari ya kuvunja rekodi ya paundi milioni 100. Madrid wanaamini uwepo wa Zinedine Zidane unaweza kuwasaidia kumshawishi Hazard kuondoka Chelsea, lakini Antonio Conte hataki kumuuza mchezaji wake.
TOLISSO KWENYE RADA ZA CHELSEA
Chelsea wanajipanga kumsajili kiungo wa Lyon Corentin Tolisso na wanaweza pia kumrejesha beki Kurt Zouma Ligue1 kama sehemu ya dili, L'Equipe kimeripoti.
OL wapo tayari kufanya mazungumzo kuhusu Bertrand Traore, ambaye anaweza kutua Ufaransa kwa euro milioni 20.
NEWCASTLE WANAMTAKA ISMAILA SARR
Kinda wa Metz Ismaila Sarr amefurahia kupata nafasi kucheza ligi kuu ya Ufaransa msimu huu na anaweza kutua Newcastle, kwa mujibu wa L'Equipe .
Rafa Benitez anataka kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 19 na timu yake imeshatoa ofa ya euro milioni 12, ingawa Metz wanataka euro milioni 15 kumwachilia.
MAN UNITED YAKATAA €60M ZA MADRID KUMUUZA DE GEA
Manchester United wamekataa ofa ya euro milioni 60 kutoka Real Madrid kwa ajili ya kipa wao David de Gea, kwa mujibu wa Sky Sports News .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akifuatiliwa sana na Real Madrid lakini United bado wamekuwa wazito kumuuza na wamesema hapana kwa mara nyingine dirisha la uhamisho linapokaribia kufunguliwa.
LEICESTER WANATAKA £50M KUMWACHIA MAHREZ
Leicester City wamedhamiria kupata fedha nono kutoka kwa Riyad Mahrez na wametangaza ada yake kuwa paundi milioni 50, kwa mujibu wa Daily Star .
Mchezaji huyo hana utulivu baada ya kampeni za 2016-17 Ligi Kuu Uingereza, lakini Mbweha hawatamwachia kuondoka kwa bei rahisi.
JUVE WANATAKA KUMSAJLI SZCZESNY WA ARSENAL
Wojchiech Szczesny huenda akaendelea kubaki Serie A msimu ujao kwani Juventus wanaandaa kitita cha paundi milioni 14 kwa ajili ya kipa huyo wa Arsenal anayecheza Roma kwa mkopo, limeripoti Daily Mail .
Mlinda mlango huyo wa Poland ameonyesha uwezo mkubwa tangu alipotua Roma, akiwawezesha miamba hao wa Italia kufuzu Ligi ya Mabingwa baada ya kumaliza nafasi ya pili.
LIVERPOOL YAMNYATIA SALAH
Wakala wa Mohamed Salah amedokeza kuwa nyota huyo wa Roma yupo mbioni kutua Liverpool baada ya kubainisha kuwa alikuwa safarini kwenda Uingereza, kwa mujibu wa Express .
MBAPPE ANATAKA KWENDA MADRID
Nyota wa Monaco Kylian Mbappe anataka kujiunga na Real Madrid licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, kwa mujibu wa Marca .
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 ametajwa kuwa kwenye rada za Man City Pep Guardiola akitaka kumweka Mbappe kwenye kikosi chake cha kwanza moja kwa moja. Lakini Mfaransa huyo anataka kutua Real Madrid na atakataa fursa ya kutua Man City.
GRIEZMANN AITAARIFU ATLETI ANATAKA KUONDOKA
Antoine Griezmann ameuambia uongozi wa Atletico Madrid kuwa anataka kuondoka majira ya joto, kwa mujibu wa Deportes COPE .
Manchester United wamekuwa kwenye harakati za kumsajili mchezaji huyo wa kimatifa wa Ufaransa, na huenda akatua kwenye kikosi hicho cha Jose Mourinho.
MOU AFANYA MAZUNGUMZO YA SIRI NA MORATA
Jose Mourinho amefanya mazungumzo ya faragha na mshambulizi wa Real Madrid Alvaro Morata, kimeripoti OkDiario .
Inadaiwa kuwa Milan ndiyo timu yenye uwezekano mkubwa wa kuipata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa dau la euro milioni 60, lakini bado Mourinho anaamini Muhispania huyo atakuwa namba 9 sahihi kwa Man United.
MILAN YATOA €60M KWA AJILI YA MORATA
AC Milan watatoa euro milioni 60 kwa ajili ya mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata kwa mujibu wa habari za La Gazzetta dello Sport
Mshambuliaji huyo wa Kihispania tayari ameshakubali kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kwa mkataba wa euro milioni 8 kwa msimu.
LINDELOF KUIGHARIMU UTD £52M
Manchester United wameambiwa watalazimika kutoa euro milioni 60 ambazo ni sawa na paundi milioni 52 kumsajili beki wa Benfica Victor Lindelof, kwa mujibu wa A Bola .
WENGER AONYWA KUHUSU USAJILI
Arsene Wenger ataonywa kuhusu tabia yake ya kusita kufanya usajili na bodi ya Arsenal katika kikao kitakachopitisha maamuzi ya kumpatia mkataba mpya leo, kwa mujibu wa Daily Mail .
Kumkosa Gonzalo Higuain 2013 ni miongoni mwa mifano ambayo Wenger alishindwa kufanya usajili ambao ulikuwa muhimu na wenye tija.
MAN UTD YAMFUATILIA BALE
Manchester United bado wanamtupia jicho Gareth Bale wakitaka kumsajili mchezaji huyo nyota wa Real madrid majira ya joto, Mundo Deportivo reports .
Ikiwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 hataanza kwenye mechi ya fainali Ligi ya Mabingwa, Meshetani Wekundu watazidi kuwa na imani ya kumsajili majira ya joto.
CHELSEA KUTUMIA £200M USAJILI MAJIRA YA JOTO
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amepewa kitita cha paundi milioni 20 kufanya usajili majira ya joto, kwa mujibu wa Daily Telegraph .
Bosi huyo anataka kuwasajili Virgil van Dijk, Romelu Lukaku na Tiemoue Bakayoko miongoni mwa shabaha yake.
RAFA ANAMTAKA REINA NEWCASTLE
Rafa Benitez anataka kufanya kazi na kipa wa Napoli Pepe Reina katika klabu ya Newcastle kwa mujibu wa The Sun .
LYON YAMTOLEA OFA CHICHARITO
Lyon wametoa ofa ya euro milioni 12 kwa ajili ya mshambulizi wa Byer Leverkusen Javier Hernandez kwa mujibu wa RMC .
Miamba hao wa Ligue 1 wanataka kuziba pengo la Alexandre Lacazette.
MAN CITY YAMTOLEA €130M MBAPPE
Manchester City wametoa ofa ya rekodi ya dunia ya paundi milioni 114 kwa ajili ya kinda wa Monaco Kylian Mbappe, limeripoti Telefoot .
MAN UTD HAITAMNUNUA PERISIC
Manchester United wamepungukiwa euro milioni 15 katika dau lao la kutaka kumsajli Ivan Perisic wa Inter Milan kwa mujibu wa Calcio Mercato
STOKE YAMTENGEA DAU ROONEY
Stoke City wametoa ofa wakitaka kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Manchester United Wayne Rooney kwa mujibu wa Daily Mirror.
Rooney alishakataa kwenda China Januari na anatarajiwa kuondoka Old Trafford msimu huu.
UTD NA CHELSEA VITANI KUMSAJILI LUKAKU
Romelu Lukaku wa Everton ameamsha vita kali baina ya Chelsea na Manchester United zinazotaka kumsajili majira ya joto.
ARSENAL YAONGOZA MBIO ZA KUMWANIA BELOTTI
Arsenal wanataka kumsajili Andrea Belotti kutoka Torrinho lakini watakumbana na ushinda kutoka kwa Chelsea na Manchester United, imeripotiwa na The Sun.
AC MILAN YAJIUNGA MBIO ZA KUMFUKIZIA DEMBELE
AC Milan imeungana na Arsenal, Chelsea na Tottenham kuiwania saini ya mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele, limeripoti Express.
GUARDIOLA KUSAJILI WATOTO WA BARCA
Pep Guardiola anataka kuwasajili vijana hatari kutoka Barcelona, Pablo Moreno, Nico Gonzalez na Ansu Fati katika timu ya Man City.
MOURINHO AISHURUTISHA MAN UTD KUMSAJILI KEANE
Jose Mourinho ameitaka bodi ya Manchester United kufanya haraka iwezekanavyo kumsajili Michael Keane kutoka West Ham united.
MORATA ANATAKA KUTIMKIA MILAN
Alvaro Morata yu mbioni kurejea Ligi ya Italia, awamu hii atatua AC Milan kwa mujibu wa Sky Sport Italia. ( via Football Italia ) .
NEYMAR NJE VERRATTI NDANI BARCELONA
Barcelona wapo tayari kuachana na Neymar ili waweze kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain Marco Verratti kwa mujibu wa Yahoo .
UNITED INAWATAKA GRIEZMANN, LUKAKU & BELOTTI
Jose Mourinho yupo tayari kutumia fedha za kutosha kuiboresha safu yake ya mashambulizi Manchester United, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mashetani Wekundu wanataka kumsajili Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, Andrea Belotti wa Torino na Romelu Lukaku wa Everton kuziba pengo la Zlata Ibrahimovic na Wayne Rooney. Beki wa Burnley Michael Keane pia yumo kwenye rada.
MOURINHO ANAMTAMANI LUCAS
Jose Mourinho anatarajia kusajili winga wa kulia majira ya joto na amemgeukia Lucas Moura wa Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa SportWitness .
Bosi huyo wa Manchester United atajaribu kwa mara nyingine kumsajili Mbrazili huyo baada ya kupata ugumu kuishawishi Chelsea kumuuza Willian.
INTER WANAWATAKA JAMES & PEPE
Inter wanataka kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa Real Madrid Pepe na James Rodriguez uhamisho wa majira ya joto, kwa mujibu wa Sportitalia .
Kadhalika Manchester United nao wametajwa kuifukuzia saini ya Mcolombia James ambaye anataka kuondoka Madrid majira ya joto baada ya kushindwa kumshawishi Zinedine Zidane.
Post a Comment