banner

July 22, 2017

JEMBE LA YANGA LATUA SINGIDA UNITED USIKU MNENE, LASAFIRISHWA KWA NDEGE

JEMBE LA YANGA LATUA SINGIDA UNITED USIKU MNENE, LASAFIRISHWA KWA NDEGE

Singida United imeendelea kujiweka sawa ambapo safari hii imenasa jembe kutoka Yanga.
Habari ni kuwa kiungo mshambuliaji Deus Kaseke ambaye alimaliza mkataba wa kuitumikia timu ya Yanga sasa ametua Singida United.
Kocha wa Singida United, Hans van Der Pluijm amezungumzia kuwa anaamini Kaseke aliyewahi kufanya kazi wakiwa Yanga msimu uliopita atakuwa na mchango kikosini kwake. 
Hadi kufikia jana Ijumaa mchezaji huyo wa zamani wa Mbeya City alikuwa katika hatua za mwisho mwisho kusaini mkataba ambapo majira ya usiku alikamilisha mipango yote na kusafirishwa kwa nmdege hadi Mwanza kujiunga na wenzake kwa ajili ya kambi.
Kaseke amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza Singida United ambako ataungana na Ally Mustapha ‘Barthez’, ambaye walicheza wote msimu uliopita Yanga na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search