banner

August 11, 2017

ALFRED LUCAS AFUNGUKA TAARIFA ZA KUFUKUZWA DODOMA KISA KUMPIGIA KAMPENI MGOMBEA URAIS

ALFRED LUCAS AFUNGUKA TAARIFA ZA KUFUKUZWA DODOMA KISA KUMPIGIA KAMPENI MGOMBEA URAIS

Baada ya taarifa kusambaa kuwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Alfred Lucas amerejeshwa Dar kutoka Dodoma kwa kosa la kumpigia kampeni mgombea wa urais, Lucas amefunguka.
Lucas ambaye kitaaluma ni mwanahabari, inadaiwa alihusika katika kumsalimia na madai mengine yakieleza kuwa amehusika katika kumpigia kampeni mgombea urais, Richard Shija.
Akizungumza juu ya hilo, Lucas alisema ni kweli amerejea Dar akitokea Dodoma kunakofanyika uchaguzi huo lakini hajafukuzwa kazi badala yake ametakiwa kurejea kufanya majukumu mengine makao makuu ya shirikisho hilo Karume jijini Dar.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search