banner

August 23, 2017

RAIS WA TFF ACHIMBA MKWARA MZITO KUHUSU WAAMUZI WA SOKA

RAIS WA TFF ACHIMBA MKWARA MZITO KUHUSU WAAMUZI WA SOKA

Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia amechimba mkwara kwa waamuzi pamoja na viongozi wa klabu ambao watahusika katika kupindisha mambo ili kuuharibu mchezo wa Simba na Yanga wa leo Jumatano.
Akifafanua zaidi, Karia amesema: “Tutakuwa wakali mno kwa wasimamizi wa mchezo huo pamoja na viongozi wa klabu ambao watajaribu kufanya njia zozote za hila ili kupata ushindi nje ya taratibu halali. Hatutasita kumpoteza mwamuzi kwenye masuala ya michezo kama ataleta mchezo na mchezo wa kesho.
“Waamuzi tuliowachagua wako makini na wanauwezo, watakapofanya makusudi yoyote na sisi, wataona makusudi yetu.”
Mechi za hivi karibuni za Simba dhidi ya Yanga zimekuwa zikimalizika huku waamuzi wakiishia kubebeshwa mizigo ya lawama kwa kushindwa kumudu mechi husika huku baadhi ya waamuzi wakiishia kufungiwa au kusimamishwa.
Kumbuka kuwa Karia ameingia madarakani Agosti 12, 2017 baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa TFF uliofanyia mkoani Dodoma.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search