banner

August 22, 2017

KOCHA AMSIFIA TSHISHIMBI ASEMA NI BORA KULIKO MKATA UMEME

KOCHA AMSIFIA TSHISHIMBI ASEMA NI BORA KULIKO MKATA UMEME

Kocha mzoefu nchini Tanzania, Joseph Kanakamfumu amemzungumzia mchezaji mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi ambaye ametua kikosini hapo hivi karibuni na kutokea kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa timu hiyo. 
Katika uchambuzi wake Kanakamfumu kayazungumza haya: 
“Mkata Umeme alisifiwa zaidi na magazeti mazoezini lakini waliomuona kwenye mechi walikuwa kila siku wakimpa muda!
“Ukimuona tu huyu Tshishimbi unaweza kukubali kuwa ni mchezaji sahihi kwa tatizo walilokuwa nalo Yanga kwa muda mrefu!
“Kwangu namuona ni bora kuliko hata Mbuyu Twite kwa nafasi ya kiungo mkabaji!
“Ana uwezo mzuri wa kunyang`anya mipira, anauwezo mzuri wa kudribble kwa kasi na kupiga pasi ndefu na fupi pale inapohitajika!
“Control yake ni nzuri na kama jana aliweza kujaribu kupiga mipira golini sawa na Mshambuliaji Ngoma wote wakipiga golini mara mbili, shuti moja likitoka nje na lingine likidakwa na kipa!
“Unaiona tofauti kubwa aliyobayo na hao kina Makapu ambao ndani ya dakika nyingi wamecheza Yanga hawajawahi hata kupiga golini, au kutembea na mipira na kupiga pasi nzuri!
“Nilichogundua ni kwamba hana mazoezi mazuri inaonekana ndio kwanza anatoka mapumzikoni!”

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search