banner

May 24, 2019

NYOTA WA SIMBA 'AWAANGUKIA' MASHABIKI NA UONGOZI

NYOTA WA SIMBA 'AWAANGUKIA' MASHABIKI NA UONGOZI


MSHAMBULIAJI wa Simba, Adam Salamba amesema kuwa kitendo chake cha kuomba viatu kwa mchezaji wa Sevilla jana hakikuwa na lengo baya bali ni 'Fair Play' kwani viatu anavyo vya kutosha.

Kwenye mchezo wa Jana uliochezwa uwanja wa Taifa na Simba kukubali kupoteza kwa mabao 5-4, Salamba alionekana akionyesha ishara ya kuomba viatu kwa mchezaji wa Sevilla.

"Haikuwa kwa ubaya mimi kufanya vile bali ni fair play, nadhani nimewakosea mashabiki na viongozi wangu wa Simba napenda kuwaomba radhi, kwani kama viatu ninavyo vya kutosha na vyenye ubora," amesema Salamba. 

Sevilla waliletwa kwa hisani ya SportPesa na walitembelea vivutio mbalimbali nchini Tanzania.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search