banner

April 03, 2020

NIYONZIMA AGOMEA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA

NIYONZIMA AGOMEA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA

HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kustaafu kucheza mpira kutokana na uwezo wake alionao ndani ya uwanja.

Niyonzima amesema kuwa bado anajua anahitajika ndani ya uwanja kwani uwezo na ujuzi unadumu.

"Kwa sasa sina mpango wa kustaafu kucheza soka kwa sasa nitaendelea kupambana ili kuwa bora na kufanya vizuri ndani ya uwanja.

"Wapo wanaotaka itokee hivyo kwangu lakini bado sijafikiria mpaka wakati utakapofika nitaamua kufanya hivyo ila sio kwa sasa," amesema. 


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search